(photo)

Karibu

Mfumo wa iHRIS ni nyenzo ya usimamizi wa rasilimali watu ambayo inawezesha shirika kubuni na kusimamia mkakati thabiti wa rasilimali watu. Wakati hapo mwanzoni ulikuwa na lengo la kusimamia wafanyakazi wa afya, Mfumo wa iHRIS unaweza kutumiwa katika mifumo mingine ya kazi. Mfumo wa iHRIS ni Maunzilaini Chanzi Huru isiyolipiwa gharama zozote iliyoanzishwa na CapacityPlus, makubaliano ya ubunifu wa kiulimwengu ili kusaidia nchi zinazoendelea kujenga na kuendeleza nguvu kazi imara.